Hatari ya Matumizi ya Bulb Hizi. - Mwl Ndiku

Saturday, 18 March 2017

Hatari ya Matumizi ya Bulb Hizi.

Tunapenda kupunguza matumizi ya nishati, hizi bulb ambazo ni rafiki wa mazingira na zinazookoa nishati(energy serving bulb) zimekuwa zikitumika zaidi kwa sasa.

Ila ni vyema ujue kwamba hizi bulb za kisasa ni kweli zina sumu. Shirika la kulinda Mazingira limetoa maelekezo ya dharura unayohitaji kuyafuata endapo bulb yako itavunjika.

Hii ni kutokana na gesi yenye sumu inayotoka endapo bulb itavunjika.

Taasisi ya Fraunhofer Wilhelm Klauditz ya Ujerumani inadai kuwa kama taa hii itavunjika ndani ya nyumba itatoa mara 20 zaidi ya Mercury katika hewa

Bulb hizi za kupunguza matumizi ya Nishati zinaweza kukuletea matatizo haya;

  • Kizunguzungu
  • Kifafa
  • Maumivu ya kichwa
  • Uchovu
  • Kutostahimili
  • Wasiwasi


1.Bulbu hizi zinazookoa nishati zina wingi wa zebaki(mercury)

Mercury ni hatari hasa kwa 

  • watoto na 
  • wanawake wajawazito. 
  • Uharibu mfumo wa neva, 
  • ubongo, 
  • figo na 
  • ini.
  • Pia uharibu uzazi, 
  • kinga ya mwili, 
  • mfumo wa mishipa ya moyo,
  • pia inaweza kukusababishia mitikisiko,
  • kukosa usingizi, kuumwa kichwa, 
  • wasiwasi na 
  • kupoteza kumbukumbu 


2.Bulb hizi zinaweza kukusababishia Kansa
  • Utafiti uliofanywa Maabara uligundua kwamba hizi balbu pia zina sumu zinazoweza kukusababishia kansa
  • Phenol, tindikali hii yenye chembechembe nyeupe zenye sumu inapatikana katika makaa ya mawe na inatumika kwa matumizi ya viwanda
  • Taa hizi zina wingi wa mionzi ya UV
  • Mionzi hii ya UV si mizuri kwa afya ya ngozi na inaweza kukusababishia kansa ya ngozi.


Baada ya kusoma haya maelezo unaweza kuchagua kuendelea kutumia balbu hizi kwa maana gharama zake ni nafuu, kama utafanya hivyo basi yakupasa kusoma maelekezo na kujua jinsi ya kukabiliana na mercury(zebaki) na kemikali zinazoweza kukusababishia kansa.

Fanya hivi kabla ya kutoa bulb iliyopasuka;


  • Watu na wanyama waondoke katika chumba
  • Fungua madirisha na milango kwa mda wa dakika 5-10