Madhara Hatari ya Pombe Mwilini na Maisha Pia - Mwl Ndiku

Tuesday, 28 March 2017

Madhara Hatari ya Pombe Mwilini na Maisha Pia

Pombe za aina ya kinywaji ambacho kinapendwa sana katika jamii, hata hivyo licha ya kuwepo kwa taarifa ya kwamba pombe huongeza furaha ya moyo,  na kuzuia matatizo yatokanayo na msongo wa mawazo, tafiti mbalimbali zinasema ya kwamba pombe zina aina zote kemikali ambazo baadhi ya hizo kemikali huwa ni katika mwili wa mwanadamu.












Labda kwa dakika chache tuangalie matatizo yatokanayo na utumiaji wa pombe.
  1. Vidonda vya tumbo.
  2. Kansa ya utumbo.
  3. Kusinyaa kwa Ini.
  4. Kansa ya Ini.
  5. Kansa ya umio(oesophagus)
  6. Vindonda kwenye mapafu.
  7. Utapiamlo hasa wale wanaokunywa huku lishe duni.
  8. Matatizo ya ganzi miguuni na mikononi(Peripheral Neuropathy).
  9. Kisukari.
  10. Figo kushindwa kufanya kazi.(Renal failure)
  11. Kansa ya figo
  12. Kukosa au upungufu wa hamu ya tendo la ndoa.(Loss of Libido)
  13. Upungufu wa nguvu za kiume.
  14. Kuongeza kasi kwa baadhi ya magonjwa hata kama unatumia dawa kama vile Kifua Kikuu,Kansa,Kisukari,Shinikizo la damu la kupanda.n.k
  15. Kukosa hamu ya kula.(Anorexia)
  16. Kutofyonzwa vyema kwa chakula(Malabosorption)
  17. Ugonjwa wa kongosho.(Pancreatis).
  18. Kichaa cha pombe(mtu hawezi kufanya kazi bila ya pombe,au anakuwa kama mgonjwa lakini akipewa pombe tu anakuwa mzima)
  19. Na pia hatari kubwa katika maisha, huongeza wimbi la umaskini kwani pesa nyingi hutumika kunywa pombe nahuku mambo ya msingi  ya maendeleo yakisahaulika.

Jambo la muhimu ni kuhakikisha unaepuka utumiaji wa pombe ila kuepuka matatizo yaliyo bainishwa hapo awali

Mungu akusaidie kuepuka hatari hiyo.

Endelea kutembelea www.mwl-ndiku.blogspot.com

No comments:

Post a Comment