1.0 UTANGULIZI
Kwa mujibu wa ibara ya
145 na 146 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali za Mitaa ni
vyombo vya haki na vyenye mamlaka ya kushiriki na kushirikisha wananchi katika
kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma katika sehemu zao.
Serikali za Mitaa huanzishwa kwa madhumuni ya kuwahudumia wananchi na
kuwapelekea madaraka kwa kuwajengea uwezo wa kiuchumi, kijamii, kisiasa na
kiutamaduni.
Sifa muhimu
zinazozitambulisha Serikali za Mitaa ni pamoja na:
i.
Kuundwa kwa mujibu wa
Katiba na Sheria.
ii.
Ni vyombo vya wananchi
ambavyo huundwa, huendeshwa, husimamiwa na kuwajibika kwa wananchi.
iii.
Hujenga demokrasia
kuanzia ngazi ya msingi.
iv.
Huleta maendeleo ya
wananchi kwani ziko karibu nao.
v.
Ni vyombo vya uwakilishi
wa wananchi katika Serikali
No comments:
Post a Comment