Baadhi ya
mboga-mboga na matunda yenye
rangi nyekundu,
zambarau na hata kijani
kibichi na njano
huwa na virutubisho kwa
wingi zaidi hasa
madini na vitamini. Baadhi ya
virutubishi hivi
huchangia sana kuongeza
damu. Mfano mmea
wa choya (rosela) ambao
una rangi
nyekundu, umeonekana kuwa na
madini chuma kwa
wingi ambayo huchangia
kuongeza damu.
Lakini haimaanishi kuwa,
kila chakula au
kinywaji chenye rangi hizo huongeza damu.
Hata hivyo
kuchanganya mboga na matunda
ya rangi
mbalimbali huongeza ubora wa chakula unachokula. Hivyo ni vizuri kujaribu
kuchanganya
rangi kadiri inavyowezekana.
Baadhi ya
mboga-mboga au matunda
vinaweza
kutumika kutengeneza supu au
v i n y w a j i
.
Watu wengi
hudhani kwamba vinywaji vya
rangi ya
zambarau au nyekundu vyenye ladha
bandia ya
matunda mfano “black curre n t ”
huongeza damu.
Hii si kweli; vinywaji hivi mara nyingi hutengenezwa na
maji, sukari,
rangi na ladha bandia,
hivyo si vizuri kuvitumia na siyo bora kwa afya zetu.
No comments:
Post a Comment