Hivi karibuni kumeripotiwa kuwepo na mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa 'kimeta' ambapo mamia ya wanyama pori katika mbuga za wanyama na wale wa kufugwa wamekufa kwa janga hilo. Hili linatukumbusha kuwa, ulaji wa nyama kwa wakati huu tulio nao ni hatari sana kulingani na magonjwa kuwakumba wanyama. Lakini,tunapaswa kujua ni virutubisho gani vinapatikana kwenye nyama na je tunaweza kuvipata wapi kama mbadala?
Nyama ina wingi wa protini. Moja ya mbadala wa nyama ni uyoga. Hebu japo kwa ufupi tuangalie umuhimu na faida ya uyoga mwilini.
Uyoga
una protini kwa wingi pia madini na
vitamini
ambazo husaidia kuboresha afya.
Ubora
wake umekaribia ule wa vyakula vya
mikunde
na maziwa. Uyoga pia
una
vitamini na madini muhimu
katika
kuboresha kinga ya mwili.
Uyoga
unaweza kutumika kama
sehemu
ya chakula kwa mtu anayeishi na virusi
vya UKIMWI. Lakini
ikumbukwe
kwamba, hakuna chakula kimoja
pekee
kinachotosheleza mahitaji yote ya
mwili
kilishe, kwa hiyo bado ni muhimu kula
chakula cha
mchanganyiko na cha kutosha.
Ikumbukwe kwamba sio kila aina ya
uyoga
inaliwa.
No comments:
Post a Comment