Chanzo cha kuabudu
jumapili.
Chanzo cha kuabudu Jumapili katika unabii Ilikuwa imetabiriwa
kwamba angemiliki mfalme ambaye angebadiri amri za Mungu (Danieli 7:25).
“Constantino, mfalme wa Rumi, alipoingia katika dini ya kikristo, alijaribu
kuunganisha upagani na ukristo, akaamuru watu wote kuadhimisha siku ya kwanza
ya juma –Jumapili (Sunday) ili siku hiyo iwekwe badala ya Sabato ya siku ya
saba –Saturday. Kumbuka kwamba Jumapili (Sunday) ilikuwa ni siku ya kawaida ya
kuabudu mungu-jua. (August Neodor, General History of Christian Religion and
Church, London, pp. 424, 425).
Constantino, Mfalme wa
Rumi (mnyama wa 4), aliweka sheria ya kupumzika Jumapili (Sunday) mnamo mwaka
321 A.C ikakubaliwa na wakristo wengi.
Alitimiza unabii wa Danieli 7:6-8. Mnyama wa nne “…alikuwa na pembe kumi (7:7).
Pembe kumi ni falme kumi: ambazo zilizotokea katika maanguko ya ufalme wa
Warumi washenzi. Na falme hizo ndio hizi: England, France, Spain, Portugal,
Germany, Switzerland, Italy, Heruli, Vandalas na Ostrogoths. (Daniel 7:24).
“Nikaziangalia sana pembe zake na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo
ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake tatu katika zile za kwanza zikang’olewa
kabisa.” (Daniel 7:8).
Uchambuzi wa unabii huu,
[A] Pembe
ndogo aliibuka kati ya pembe kumi za mnyama huyo (yaani falme kumi 10) –Daniel
7:8, 24-25. Jambo hili lilianza taratibu katika kipindi cha mfalme CONSTANTINO
alipofanya maridhiano na SILVESTA aliyekuwa kiongozi wa kanisa mnamo mwaka wa
313-321 AC. Jambo hili likawa endelevu hata Askofu wa Rumi akapewa mamlaka ya
kutawala makanisa yote na serikali zote (476 AC).
[B] Ufalme huu ulipoanza, falme
tatu zikang‘olewa. Ndizo hizi: HERULS, VANDALAS na OSTROGOTHS wakaangushwa
wakijaribu kupambana na utawala na uwezo wa Kanisa la Rumi. Shabaha ya ufalme
wa pembe ndogo, yaani Upapa, ilikuwa kuimalisha Kanisa la Katholiki, kukuza
mamlaka ya Papa na kuadhimisha siku ya ibada ya jua, yaani Jumapili (Sunday),
kama ishara ya utawala huo wa pembe ndogo. „Kama ishara ya mamlaka ya Kanisa la
Katholiki, waandishi wa Upapa wameandika kwamba ‚Kitendo cha kubadiri Sabato na
kuweka Jumapili, ambacho Waprotestanti wanakubaliana nacho kwa kupumzika
Jumapili, wanatambua mamlaka ya Kanisa ya kuongoza sikukuu, na kuwahukumu kama
wadhambi wale wasiotii. Hivyo kubadilishwa kwa Sabato (amri ya nne) ni nini
kama siyo alama au ishara ya mamlaka ya Kanisa la Rumi, yaani ‚Alama ya
Mnyama‘?“ (Great Controversy, p. 448; Tragédies des siècles, p. 485. Haya
yameandikwa na H. Tuberville, katika kitabu chake „An Abridgement of the
Christian Doctrine, p. 58“).
[C] Atawadhoofisha (yaani kuwatesa) walio
watakatifu (Danieli 7:24-25). Katika historia ya ulimwengu hakuna taifa wala
ufalme uliowahi kuwatesa na kuwauwa watakatifu wa Mungu kama kanisa la Roman
Catholic. Ndiyo maana hata vitabu vya kanisa Katoliki vinathibitisha utimilifu
wa unabii huu kwa maneno ambayo Papa Martin V (1417–1431 A.C) aliyotoa kwa
mfalme wa Poland kuhusiana na wakristo wa kweli waliokuwa wafuasi wa JOHN HUSS
akasema; “Hakikisha kama unawaangamiza wafuasi wote wa HUSS… choma, ua kwa
wingi fanya kila mahali pawe jangwa kwani hakuna jambo linalokubalika zaidi kwa
Mungu, au linalofaa zaidi katika wajibu wa mfalme, kama vile kuwaangamiza
wafuasi wa HUSS.“ (L.M. de Comentin, The public and private History of the
Popes of Rome, Vol. III, p. 116,117). - Pumziko la Jumapili ni alama ya Upapa,
yaani „alama ya mnyama“ - Papa hujiita anayesimana mahali pa Kristo (Vicarius
Filii Dei) - Katika siku za mwisho, Marekani (USA) itatetea pumziko la Jumapili
- Umoja wa madhehebu (WCC), yaani sanamu ya mnyama, inaandaa vita vya mwisho
dhidi ya Sabato ya kweli - Kuadhimisha pumziko la Jumapili ni chanzo cha mateso
ya watakatifu wa Mungu - Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila
ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo…
(Ufunuo 13:8, 11-18).
Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi
nyote. Amina.
Habari zaidi kuhusu masomo haya;
Namba, +255758924982, +255714697526.
E-mail ndiku.live@outlook.com
Facebook; Mwl Ndiku
No comments:
Post a Comment