PEMBE NDOGO YA DANIELI 7.
Pembe ndogo katika
kitabu cha Danieli;
Je!
Ni kitu gani? Je! Tunaweza kuitambua kwa ufasaha? Je! Historia inaweza ikathibitisha
unabii uliotabariwa katika Biblia?
Kabla hatujaanza kuangalia hiyo pembe ndogo
huashilia nini, je! unabii hueleza ‘pembe’
kama kitu gani? Tunapaswa kulifahamu kwanza hili kwa sababu Maandiko husema
kwamba, “Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko
upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu”. 2Petro 1:20. Hiyo humaanisha kuwa sipaswi kukueleza mawazo
yangu juu ya kile kinachoashilia unabii. Ninapaswa kuiacha Biblia ndiyo ieleze
kuhusu unabii.Bila shaka hii inakuwa ndiyo njia pekee ya kuwaumbua manabii wa
uongo. Ni rahisi sana. Wewe sikiliza kile wanachokisema, na kisha fanya
uchunguzi juu ya kile wasemacho ukilinganisha na neno la Mungu. Bwana amekwisha tuelezea ishara zote
za kiunabii! Hivyo basi, maandiko hutueleza nini kuhusu pembe?
·
Danieli 7:24, “Na
habari za zile pembe kumi, katika
ufalme huo wataondoka wafalme kumi;
na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye
atawashusha wafalme watatu.”
·
Danieli 8:21, “Na
yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.”
·
Ufunuo 17:12, “Na
zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme
bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule
mnyama.”
Kutokana na maandiko ya kiunabii hapo juu, pembe=mfalme.
Kama umekwisha soma kitabu cha Danieli sura ya pili, utakuwa
unafahamu ile njozi katika sura hiyo ambayo ilitabiri falme kuu za dunia zitakazokuwepo na ufalme
tunaouona kwa sasa.
·
Danieli 7:2,3.
“Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na
tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. Ndipo
wanyama wakubwa wanne wakatoka
baharini, wote wa namna
mbalimbali.”Katika hii njozi, wanyama wakuu wanne,(wanyama=mataifa.
Angalia Danieli 7:23) walitokea mmoja baada ya mwingine, ikiashiria kutokea kwa
falme kuu katika dunia. Hawa wanyama
wanne huwakilisha falme zote kuanzia wakati wa Danieli ambapo ndipo wakwanza ulianza (Babeli) hadi
ufalme wa mwisho (Rumi) utakaokuwepo
hadi siku ya mwisho .
·
Danieli 7:7, “Baadaye
nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye
nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana;
alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na
umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.”
·
Danieli 7:23,24 " Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne
juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na
kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande.Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa
mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.
Tumeona kwamba zile pembe kumi ziliota kwenye yule mnyama wa mwisho, huyu mnyama
anaeleweka vizuri ambapo hata vitabu vya kihistoria hutaja kuwa ni Rumi. Hizi pembe kumi uhalisia ni kwamba zinawakilisha
kugawanyika kwa ufalme wa Rumi katika mataifa kumi baada ya ufalme huo kuanguka
mnamo mwaka 476BK.
Wakati Rumi imeanguka
iligawanyika katika mataifa kumi:
|
|
Ikumbukwe kwamba hakuna “ mnyama” mwingine anayeonekana
kutokea katika unabii baada ya yule wa nne. Rumi ya kipagani pamoja na Rumi ya
kidini ndizo falme kuu za mwisho zilitajwa katika unabii.
Sasa tumefika katika kiini cha somo hili. Danieli sasa
anazungumzia PEMBE NDOGO ambayo imezuka kutoka kwenye hizo pembe kumi. Kumbuka,
pembe ni wafalme waliopata nguvu baada ya Rumi kugawanyika. Muda mfupi tutaona
kwamba pembe ndogo ilizuka kutoka kwenye
zile pembe kumi na itapokea nguvu ya mnyama wa nne ambaye ni wa
mwisho.
·
Danieli
7:8,”Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati
yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza
zikang'olewa kabisa; na tazama, katika
pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa
kikinena maneno makuu.”
·
Danieli 8:9,10 “Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe
ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande
wa nchi ya uzuri. Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni;
ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga.”
Haya mafungu yanazungumzia kukua kwa mamlaka ya mwisho, inayowakilishwa na pembe ndogo. Kwa
maelezo zaidi kuhusu pembe hiyo ndogo, hebu tutazame namna unabii unavyo
ieleza.
Vigezo tisa(9) vya
kutambua pembe ndogo ya Danieli 7.
|
|
Danieli 8 iatupatia
vigezo 9 zaidi!
|
|
Kwa msaada wa vigezo hivyo
18 vya unabii wa neno la Mungu, na ushahidi unaothibitika kihistoria,kila mmoja
anaweza sasa kugundua pembe ndogo ni nini. Na ndiyo maana biblia ni tishio
kubwa sana kwa kanisa la Romani Katholiki.wanajua kwamba watafichuliwa na
maandiko matakatifu ambayo huendana kabisa na jinsi matukio ya kihistoria
yailivyo .Na ndiyo maana miaka iliyopita RC ilifanya iwezavyo ili kuficha
biblia hata isipatikane mikononi mwa watu. Baada ya uvumbuzi wa
uchapishaji,walijikuta hawawezi kuificha tena. Hivyo waliamua kupotosha
maandiko kwenye biblia katika juhudi za
kuficha ukweli. Na ndiyo maana leo hii unaona biblia za kishenzi ambazo kweli
ya Mungu imetupiliwa mbali au imebatilishwa.
Hata hivyo mwovu hawezi kuruhusiwa kabisa kufuta kweli yote ya
Mungu katika mandiko matakatifu. Mpaka sasa Biblia yenye usalama kwa kipindi hiki,ambayo
ina mapungufu madogo tena ambayo mengi
yao ni katika matumizi ya “alama za uandishi” ni biblia ya “King James”. Mungu
atukuzwe kwa kulilinda neno lake kwa ajili ya wamchao. Litukuzwe jina lake kwa
kuwa bado tunaweza pata mafundisho na mahusia ya Mungu kama neno lisemavyo; “Elekeza
moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.”
Mithali 23:12.
Kwa hivyo basi hata ukichunguza vitabu vya kihistoria ukaangalia
na sifa za ile pembe ndogo hakuna kitu kingine isipokuwa ni Upapa ndio
unaoendana na sifa hizo kwa uhakika.
Jambo moja la msingi mpaka hapa tulipofikia katika somo hili ni
kwamba,pembe ndogo huwakilisha mfumo wa kipapa na siyo ndugu zetu wapendwa
wakatholiki ambao wamenaswa katika huo mfumo. Laiti kama tungewachukia
wakatholiki kama watu wengi wafanyavyo, basi pasingekuwa na haja ya kuwaandikia
haya yote kwa nia ya kuwaonya na kuwaonesha siri ya uasi. Shetani siku zote
anapotosha ukweli ili kufanya uongo wake uonekane kama ukweli. Ama kwa hakika
wenye maarifa ya Mungu huuona oungo huo na kuukemea.
Ndugu yangu ukweli ni kwamba kuna watu wengi wako chini ya mfumo
wa kipapa na huku wanampenda Yesu Kristo kwa moyo wao wote. Bwana alijifanya haoni katika zama za ujinga,
ndivyo ilivyo leo kwamba atatuhukumu kulingana na nuru tuliyopewa. Kwa
mantiki hiyo tuwaombee ndugu zetu wa kanisa la Romani katholiki. Tuwaombee ili
kwamba waweze kusikia ujumbe wa Mungu na kutii wito wa Yesu usemao “tokeni
kwake enyi watu wangu” kabla muda haujaisha.
·
Yahana 10:16, “Na
kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na
sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja”.
Hebu hili lieleweke vizuri; Mungu anawapenda sana wale wote
waliotekwa kwenye mtego wa mfumo wa kipapa. Ndiyo maana ametupatia neno lake
ili kwamba tulisomapo, tufahamu maonyo yake
na kuwa tayari kuitikia wito wa Yesu ili kukimbia huo mfumo na kuingia
katika zizi walimo kandoo wa Bwana.
Mambo kadha wa kadha yametendwa na kanisa la RC kufanya watu waendelee
kutekwa na kuwa chini ya mfumo huo wa kipapa.
Miongoni mwa mambo yaliyohafifisha maisha ya kiroho ni lile la
mwaka 1229BK.
Fundisho hilo lililetwa na halmashauri ya Valensia, kulenga zaidi
biblia iwe miongoni mwa vitabu vinavyo
zuiliwa vikali kutumiwa na watu. Fundisho hilo lilikuwa na madai kuwa;
“ ni marufuku kwa mtu wa kawaida kusoma agano la
kale wala jipya. Wakuu wa wilaya
watahusika kuwatafuta kwa umakini wazushi wote katika makazi yao na hata
mafichoni ili kuwashughulikia kikamilifu”. Council Tolosanion, Pope
Gregory IX, Anno.Chr.1229.
|
Vatican inatambua vyema kuwa Biblia inaweza kufichua siri zote
zinazotendeka humo. Hivyo ilifanya juu chini ili kuhakikisha Biblia haipatikani
kwa waumini. Mbaya zaidi ni kwamba watu wengi waliuawa kikatili kwa sababu
walikataa kukana kweli walizokuwa wamezisoma katika biblia zao. Na hiyo nayo ni
moja ya sifa za hiyo pembe ndogo kama tunavyoshuhudia hapo chini.
Hebu tujikumbushe sifa chache za pembe ndogo tuone kama kweli
zinapatana na upapa. Hebu tuone namna biblia inavyoifichua hiyo mamlaka kama
mpinga Kristo.
·
Danieli 7:8
“Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao,
nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza
zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho
ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.”
·
Ufunuo 13:4 “Wakamsujudu
yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule
mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye
kufanya vita naye?”
Kama tulivyoona awali,wakati Rumi ilipoanguka, iligawanyika katika
mataifa kumi yanayojitegemea. Na kulingana na huu unabii, kuna mtu atapokea
nguvu baada ya huu mgawanyiko. Je, hili lilitokea? na kama lilitokea, ni nani
basi aliyepokea nguvu ya huyu mnyama wa nne ili kuendeleza ukatili wake dhidi
ya Ukristo? Je! Tunajua kuwa Rumi iliua Wakristo wengi na kuwatenda vibaya? Na
je! Ni nani aliyetawala baada ya Rumi
kuanguka?
“Miaka mingi
iliyopita, wakati Rumi ilipotelekeza falme za magharibi ilibaki kwa huruma za
wenjeji wake,warumi walimgeukia mtu mmoja tu awe msaada na ulinzi na
kumwambia awatawale,..na hivyo ikawa ndiyo muda wa kuanza kwa kutawala kwa
mapapa .Na kwa upole akakikalia kiti cha
enzi cha ukatili, mwakilishi wa Kristo akainuliwa ambaye watalawa na
wafalme wa Ulaya wanapaswa kumsujudia kwa heshima….” American Catholic Quarterly Review, April, 1911.
“Mbali na
kuvurugika kwa kisiasa huko Rumi,
paliinuka mamlaka kuu na yenye nguvu ya Kanisa la Roma.”—A..C. Flick, The Rise of the Mediaeval Church, 1909, p. 150.
“Chini ya Ufalme wa Rumi, mapapa hawakuwa
na utawala huru. Lakini wakati Ufalme wa Rumi ulipogawanyika na kuwa na
watawala mbalimbali, wenyeji wa falme hizo, kanisa la Romani Katholiki
haikuwa tu huru kama taifa katika maswala ya kidini, lakini pia ilitawala na
mambo mengine nje ya kidini. Kwa nyakati tofauti tofauti, chini ya watawala
hao kama Charlamagne (768-814),(Otto the Great (936-973), na Henry III
(1039-1056) nguvu ya umma iliongoza kanisa kwa kiasi fulani;lakini kwa
ujumla, chini ya mfumo wa siasa duni ya umwinyi, kanisa lililokuwa
limejijenga vizuri, likiwa na umoja na lenye msimamo,likiwa na papa juu yake,
halikuwa tu huru katika mambo ya kidini lakini pia liliongoza na mambo ya
kijamii”._Carl Conrad
Eckhardit, The Papacy and World-Affairs, The University of Chicago Press,
1937, p.1.
Papa Pius ix, utawala wake (I., p. 253), alisema: “Mtawala anaye ongea nanyi kwa sasa, ndiye
pekee mnaye paswa kumtii na kumwamini.”
(Tukizungumzia wakati,yapata mwaka wa 500BK, wakati Ufalme wa
Rumi ulipogawanyika katika vipande),
“Haiwezekani kanisa Katholiki kufikia mwisho kwa namna yoyote. Ndilo lenye
kuendeleza utawala…kwa baadaye ufalme wa pili utainuka, na kwa huu ufalme
papa ndiye atakuwa na mamlaka—zaidi ya
hili,ndiye atakuwa na mamlaka juu ya Ulaya nzima. Naye ataamrisha matakwa
yake kwa wafalme ambayo watayatii.”—Andrea Lagarde, The Latin Church in the Middle Ages, 1915.p. vi.
|
Uhalisia
wa kihistoria ni kwamba, utawala pekee ulioinuka ukiwa na nguvu ya kirumi, au uliozuka
ndani ya mataifa kumi muda mfupi baada ya kuanguka kwa Ufalme wa Rumi kwa
hakika ulikuwa ni mfumo wa upapa. Kwa kutumia fikra ya kawaida, jiulize kwa nini linaitwa Kanisa la Romani
Katholiki? Siyo tu mfumo wa upapa
uliridhika na malmaka, bali ulikubali jina pia. Cha kushangaza zaidi kati ya hayo
yote ni kwamba kanisa la Romani Katholiki linakiri kuwa ndilo lililofuata baada
ya kuanguka kwa Rumi kuwa na mamlaka.
“Kwa amri ya mamlaka takatifu, pale
ulipoanguka Ufalme wa Rumi na kugawanyika katika falme zinazojitegemea, papa
wa Roma, ambaye Kristo mwenyewe alimfanya kuwa kichwa na mwamba wa kanisa lake,
alipokea mamlaka ya serikali ya kijamii”.-papa Pius IX, Apostolic Letter Cum Catholica Ecclesia, March
26, 1860.
|
Pembe
ndogo ilizuka baada ya mataifa kumi kuundwa, yaani baada ya mwaka 476BK, ndio
mwaka ambapo mgawanyiko wa Ufalme wa Rumi ulikamilika. Historia hutuonesha kuwa
upapa wa Romani katholiki uliingiza utawala wa kidini na kisiasa kuanzia mwaka 538 BK, na kuendelea. Hiyo ni
takribani miaka 60 baada ya pembe ndogo kupokea nguvu.
·
Danieli
7:24, “Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme
huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa
mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.”
Hili fungu linaeleza kuwa pembe ndogo itakuwa tofauti na yale
mataifa kumi yaliyo itangulia.Ukiangalia mfumo wa kipapa, jambo hilo linaweza
kuthibitika kirahisi kwa kuwa upapa umejikita na siasa na dini, kitu ambacho
hakijawahi kutokea tangu dunia kuumbwa kwa taifa kuchanganya dini na siasa kwa
wakati mmoja. Kwa hiyo Danieli aliliona jambo hilo miaka mingi iliyopita kuwa
litatokea. Na Ufunuo 17:3 inathibitisha
njozi aliyoiona Danieli.
·
Ufunuo 17:3, “Akanichukua
katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu
sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”
Ninatumaini kuwa mpaka sasa unatambua vyema pembe kumi za mnyama, na
sifa zingine zinazooana na zile za pembe ndogo. Likini jambo lakushangaza hapa
ni kwamba mwanamke amekalia mnyama mwekundu. Hii humaanisha nini? Katika unabii
tumeshajifunza kuwa mnyama humaanisha taifa. Lakini pia, ulikuwa unafahamu kama
mwanamke katika unabii huamanisha kanisa?
·
Yeremia 6:2, “Binti
Sayuni aliye mzuri, mwororo, nitamkatilia mbali.”
·
2Wakorintho 11:2,
“Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili
nimletee Kristo bikira safi. “
Tunafahamu
kuwa kanisa la Yesu Kristo linatambulika kama bibi arusi kama maandiko yanavyotueleza. Sasa tuangazie Rumi, hiki
kinachoelezwa kinathibitika moja kwa moja kuwa kanisa na taifa kwa wakati
mmoja! Jambo hili halijawahi kutokea.
·
Danieli
7:20, “na habari za zile pembe kumi zilizokuwa
kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka
pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari
kuliko wenzake”
Katika
fungu hili la kiunabii, tunaona mwonekano wa ajabu na ulio hodari kuliko zile
zingine. Upapa wa kanisa katholiki tangu mwanzo hadi sasa umekuwa na mwonekano wa kuvutia sana
kwa macho kuliko mamlaka yoyote duniani. Mwonekano huo iliurithi kutoka kwa
Rumi ya kipagani. Kiuhalisia, mapapa wamekuwa wakijikweza kwa kiburi katika
matendo yao na misafara kama vile vile afanyavyo mtawala na wapambe wake.
Haijalishi kama ni kusanyiko dogo
linalofanywa na kanisa hili au liwe kubwa utashuhudia mapapa wamejaa mavazi ya
kiburi na ya kipagani huku wamezungukwa na watu maarufu na matajiri na kundi
kubwa la watu hali inayoonesha kuwa watu wanatoa sifa kwa mtu badala ya Mungu kama maandiko yalivyotabiri
kuwa watu wataabudu na kusujudia kiumbe
badala ya Muumba katika siku za mwisho.
·
Danieli
7:8, “Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama,
pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe
tatu katika zile za kwanza zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo
mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno
makuu.”
Andiko
hili la kiunabii linatuonesha kwamba juu ya upapa ataketi mtu mmoja; yaani
papa. Na huyu huchukuliwa kama mtu
asiyekosea na mwenye mamlaka ya kuamuru chochote na ni lazima kitekelezwe.
“Mamlaka
ya papa haina mwisho,na ni isiyozuilika; inaweza kuharibu na kumpoteza
yeyote,
kama Innocent III alivyosema.Papa anaweza kumwadhibu mtu yeyote, na mamlaka
yake hairuhusu kukata rufaa maana ndiyo ya mwisho katika utendaji; kwa maana
papa ndiye mwenyemamlaka zote katika kifua chake kama alivyosema Boniface
III.Na kwa kuwa hawezi kukosea, basi yeye ndiye mwamuzi wa kila jambo katika
kanisa kwa kutunga miongozo, kuleta
kila aina ya fundisho, kuamrisha kila aina ya matakwa yake katika maswala
mazima ya imani. Hakuna haki yoyote inayoweza kusimama kinyume yake ikiwa ni
ya mtu binafsi au shirika”
Ignaz von
Dollinger, “A Letter Addressed to the Archbishop of Munich” 1871; as quoted
in MacDoudall, The Action Newman
Relations (Fordham University Press) pp.119,120.
|
Ile kusema kwamba Papa hakosei, maamuzi yake
huathiri mabilioni ya watu ulimwenguni. Na kwa muda mwingi, utawala wa upapa
umekuwa umejawa na kiburi na kuwa
kinyume hata na Mungu aliye juu. Kwa kulitafakari andiko hilo hapo chini,
mapapa huongea maneno makuu.
·
Daniel
7:8, “Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama,
pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe
tatu katika zile za kwanza zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo
mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno
makuu.”
·
Danieli 7:24, “Na
habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na
mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu.”
Kama ilivyoelezwa awali, upapa ulifaulu kizing’oa falme tatu kati
ya yale mataifa kumi ambayo yalipinga kuwepo kwa mamlaka ya upapa. Rumi
ilihitaji sana kubaki katika madaraka, na itakuwa hivyo kwa namna yoyote ile
kwa kumteketeza yeyote atakayeingia kwenye njia zake.
Kwa mfano;
·
Heruli, iling’olewa
kabisa mnamo mwaka 493 BK.
·
Vandali, iling’olewa
rasmi mnamo mwaka 534 BK.
·
Na Ostrogothi,
ilikuwa ya mwisho kung’olewa mnamo mwaka 538 BK.
“Vigilius…
alikikalia rasmi kiti cha upapa mnamo mwaka (538 BK)chini ya ulinzi wa kijeshi wa Belisarius” History of the Christian Church, vol. 3 p. 327.
|
Kulingana na historia,
mwaka 538 BK, ndipo upapa uliaanza rasmi kuwa na mamlaka kule Ulaya ukiwa kama
kanisa na taifa kwa wakati mmoja, au “mwanamke juu ya mnyama” kama
ilivyotatajwa kwenye Ufunuo. Ukweli ni kwamba, upapa umetawala mambo mawali,
siasa na dini na ndiyo maana hauko tayari kuachia enzi yake hata kama ni kwa
gharama gani! Ndiyo maana unabii hutueleza kuwa;
·
Danieli 7:20, “ na
habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine
iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye
macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko
wenzake.”
·
Danieli 7:25 “Naye
atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake
Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake
kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.”
·
Danieli 8:25, “Na kwa
mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake
moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye
atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya
mikono.”
Kiburi cha upapa kinaelezwa katika Danieli 7 na 8 kuwa si cha kawaida.
Lakini kiburi si kwamba ndiyo zaidi kwa
maovu yanayotendwa na upapa, la hasha!, haja yake kubwa ni kukanyaga na
kumpoteza yeyote anaye kwenda kinyume na matakwa yake. Na hata umeweza kuthubutu kujitwika utukufu na uweza wa Mungu aliye juu na hata
kutenda mambo mengi ya makufuru juu ya Muumba wa mbingu na nchi.
Je! Vatican imeyatenda hayo?
·
Yohana 10:33,
“Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa
kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu.”
·
Marko 2:7, “Mbona
huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja,
ndiye Mungu?
Kutokana na neno la Mungu,
matendo haya mawili humanisha kukufuru;
·
1.Mwanadamu kujifanya
ni Mungu.
·
2.Mwanadamu
kumwondolea dhambi mwanadamu mwenzake.
Je! Upapa unayafanya mambo hayo?
“Papa ni mwenye
heshima na enzi yote, hivyo si mtu wa kawaida,…. Yeye ni kama Mungu angekuwa
duniani, ndiye mwaminifu pekee wa Kristo, ni mfalme wa wafalme, mwenye
mamlaka kamili.” Lucius Ferraris, “Promta Bibliotheca”,
1763, volume VI.p.25-29.
“Mwalimu mkuu katika kanisa ni papa. Hivyo, watu wote wanapaswa
kunyenyekea na kutii matakwa ya kwanisa na ya papa, kama kwa Mungu mwenyezi.”
–On the Chief Duties of Christians as Citizens- Encyclical letter, 1890.
“Hivyo papa
amevikwa vilemba vitatu, kama mfalme wa mbingu, wa nchi na wa kuzimu.” Lucius
Ferraris, Prompta Bibliotheca-, 1763, volume VI,
‘papa II’, P. 26.
|
Ama kwa hakika inashangaza sana, na mbaya zaidi upapa umejiweka kuwa
Mungu hapa duniani. Lakini kwa kusema
kuwa Papa ni mfalme wa mbingu, iko wazi kabisa kuwa anajitambulisha upande wa
shetani, ambaye alihitaji sana kuwa kama Mungu aliye juu; Isaya 14. Ni mpinga
Kristo pekee awezeye kutenda mambo ya makufuru, na haya ndiyo yanayomjaza
shetani moyo!
·
Isaya 14:12-15,
“Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi!
Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
Nawe ulisema moyoni
mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za
Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za
kaskazini.
Nitapaa kupita vimo
vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye
juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo”
Maandiko humfunua mtu yule aliyeko Roma (Papa) kuwa ndiye anaye
fanya kama yale ayafanyayo Lusifa, malaika aliye angushwa ambaye ndiye Shetani.
Hili fungu linaendana kabisa na maneno ya majivuno ya mapapa wanayoyasema tena
linatosha kabisa kuthibitisha na majigambo yao.
Sasa huo ukatili utakaa Roma kwa muda gani? Kulingana na unabii,
upapa ndio unaokwenda kuwakabili wakristo popote pale walipo. Kama wewe ni
Mkristo uliyetajwa katika Ufunuo 12:7,
jiandae kuteswa vikali kwa sababu vita ya pembe hiyo iliyo ndogo (upapa) ni kwa wacha Mungu wanaokataa
mafundisho potofu ya upapa. Maandiko yanatueleza;
·
Danieli 7:21,
“Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda;”
·
Danieli 7:25, “Naye
atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake
Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake
kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.”
Kwa hiyo maandiko yanaonesha kuwa pembe ndogo ndiyo yenye
kuwakabili watu wa Mungu aliyejuu. Uhalisia ni kwamba, historia inaeleza kuwa
upapa uliua watu wengi sana wakati ulipoinuka hadi zama za kati, zaidi ya wale
aliowaua Adoph Hitler wakati wa vita ya pili ya dunia. Ukweli ni kwamba, upapa
uliua watu mara 25 kwa wale aliowaua
Hitler. Sijui Romani katholiki ina nguvu ya namna gani, maana hadi sasa watu
bado hawajagundua maovu hayo na wanazidi kuiamini tena kwa kicho! Tena historia
huonesha kuwa upapa takribani watu milioni 150 waliokataa mamlaka ya upapa
waliuawa kikatili.
“Kanisa la Roma
limemwaga damu nyingi isiyo na hatia kuliko taasisi yoyote iliyowahi kuwako
duniani”—W.E. Lecky. Rise
and Influence of Rationalism in Europe. Volume 2. p. 32.
“Kwa kufundisha
imani tofauti na ile inayofundishwa na kanisa la Romani Katholiki, historia
imerekodi kuwa, mashahidi wa Kristo zaidi ya milioni 100 waliuawa” . Brief Bible Readings p.16.
|
Ama kwa hakika Kanisa la Roma limemwaga damu ya watu wengi sana na
kuwatesa vibaya wale wote waliokataa kukubaliana na matakwa ya upapa. Kwa
kufahamu zaidi namna upapa ulivyo tenda ukatili soma kitabu hiki “FOXES’S
BOOK OF MARTYS”, au wasiliana nami kupitia E-mail hii ndiku.live@outlook.com nitakutumia na vitabu vingine zaidi. Pia waweza kusoma makala
hii; March 27, 2000. Truth Provided News letter, inayomhusu papa John
Pual II, akikili hatia ya mauaji ya roho za watu na ukatili ulio fanywa na
makadinali wengine ukiwemo utoaji wa mimba.
·
Danieli 7:25, “Naye
atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake
Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake
kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.”
Katika fungu hili, tunaona kuwa pembe ndogo (upapa) italazimu
kubadili majira na sheria za Mungu. Je! Upapa umeyatenda hayo?
Ukweli ni kwamba, upapa uliondoa amri ya pili ya Mungu inayokataza
kusujudu na kutumia sanamu; katika kanisa la Romani Katholiki, zimo sanamu nyingi
ambazo hata wanazipigia magoti na kuzisujudu. Sasa kwa kuwa wamefuta amri ya
pili, ilibidi waigawe amri ya kumi ili zitimie kumi. Hiyo ni kuhusu amri za
Mungu, vipi kuhusu majira?
Upapa umediliki hata kukili kuwa ulihamisha siku ya kupumzika
Jumamosi kwenda Jumapili. . Na pia amri ya nne inayohusu sabato ilipotoshwa
mantiki yake na watu wakadang’anyika, sasa badala ya “ Ikumbuke siku ya sabato uitakase” Kutoka
20:8, kanisa hilo ovu limepotosha na kusema “Shika kitakatifu siku ya Mungu”.
Hivyo ndivyo fungu la danieli 7:25 lilivyotimia.
Historia inaeleza hivi:
“Papa anayo mamlaka
ya kubadili majira, kufuta amri, na kufanya chochote hata kama ni agizo la
Kristo”--- “Papa anayomamlaka kufanya chochote hata kama kiko kinyume na
Kristo”. Decretal de
Translatic Episcop. Cap. ( Papa anaweza kukosoa sheria takatifu.) Ferraris’
Ecclesiastical Dictionary.
“Kwa kweli kanisa
Katholiki linakili kuwa lilihamisha Jumamosi kwenda Jumapili. Na tendo hilo
huonesha mamlaka yake katika mambo ya kidini.” H.F. Thomas, Chancellor of Cardinal Gibbons.
“Jumapili ni ishara
ya mamlaka yetu…… kanisa liko juu ya Biblia, na hili la kubadili utunzaji wa
sabato ndio uthibitisho wa kauli hiyo.”
Catholic Record of
London, Ontario Sept 1,1923.
|
Hebu ona huo ujasiri wa kutamka mambo mazito kiasi hicho! Unabii
unaeleza kuwa pembe ndogo itabadili majira na sheria, ni jambo ambalo hata
Vatican yenyewe hujigamba kuwa, “Papa anayo mamlaka ya kubadili majira, kufuta sheria...” Ukweli ni kwamba, mtu kuvamia amri ya nne na
kuibadili inathibitisha kikamilifu unabii huu. Kwa sababu amri hii ya nne siyo
tu kuwa ni amri, bali pia ni amri
inayohusu muda ambao Mungu mwenyewe
ameweka kuwa siku ya pekee ya kuabudu.
Katika maandiko, tunaendelea kushuhudia nini?
·
Danieli 7:25, “Naye
atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake
Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake
kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.”
Fungu hili linaonesha kuwa watakatifu watatiwa mkononi mwake kwa
wakati,nyakati mbili na nusu wakati. Sasa nini maana ya wakati, nyakati mblili,
na nusu wakati? Kabla hatujaendelea mbele, hebu tuaangalia kwanza jinsi maeneo
mengine ya kiunabii yanavyolieleza jambo hili. Ufunuo 13:5, huzungumzia jambo
hili kama miezi arobaini na miwili (42)
·
Ufunuo 13:5, “Naye
akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya
kazi yake miezi arobaini na miwili.”
Miezi arobaini na miwili ya Ufunuo 13:5, na wakati, nyakati mbili
na nusu wakati katika Danieli 7:25 ni kitu kimoja. Uhalisia ni kwamba, miezi
arobaini na miwili ni sawa na “miaka 3
½.” Je, hili linaleta mantiki ukilinganisha na
Danieli? Wakati (mwaka mmoja) na nyakati
mbili (miaka miwili) na nusu wakati (nusu mwaka) kiukweli ni sawa miaka mitatu na nusu,au miezi 42 (12+24+6+=
miezi 42) kwa hiyo inakubali kabisa na hoja ile ya kwa Danieli. Ukichukua na
Ufunuo 12:6, inathibitisha kwa ufasaha kabisa kwamba kanisa la Yesu
litakimbilia nyikani kwa muda wa siku 1260 wakati pembe ndogo itakapokuwa inaua
Wakristo.
Ukweli ni kwamba, miezi 42, au miaka 3 ½ ni sawa na siku 1260.
Lakini mtu ataendelea kujiuliza kuwa miezi 42 mbona si sawa na
siku 1260 kwa sababu miezi yote haina siku 30. Na kama ukizidisha mara siku 365
za mwaka kwa 3 ½ ,huwezi kupata 1260, badala yake utapata 1277.5. Ndugu yangu uhalisia
kuhusu mwezi katika biblia huhesabiwa kwa kuzingatia mzunguko wa jua; yaani,
(mwezi 1= siku 29.56 ambayo ikikaribishwa kwa makumi yaliyo karibu ni sawa na
30.) Ki ukweli hata wayahudi halisi hadi sasa bado wanatumia mfumo huu
wanapozingatia sherehe zao na matukio mbalimbali.
Sasa ili kufahamu vizuri kuhusu miezi 42, au wakati, nyakati mbili na nusu wakati ambayo
pembe ndogo itatawala, ni lazima kwanza tutafute namna biblia inavyosema
kuhusu muda unavyohesabika. Mungu
anasema ;
·
Ezekieki 4:6, “Tena
utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa
nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku
moja kwa mwaka
mmoja, nimekuagizia.
Na pia tunaona kuwa Biblia hutambua mwezi mmoja kuwa ni siku 30.
Kwa sababu katika kitabu cha Mwanzo 7:11 tunaona kuwa mvua ilianza kunyesha
siku ya 17 ya mwezi wa pili, na katika Mwanzo 8:3,4 tunaona kuwa maji yalikauka
kwa muda wa siku 150. Kisha Biblia husema kuwa safina ilitua chini siku ya 17
ya mwezi wa 7, ambayo sasa ni miezi 5
kamili. Na kama ukigawa siku 150 kwa miezi 5 utapata siku 30 kwa kila mwezi.
Kwa hiyo mtazamo wa kibiblia hutambua mwezi 1= siku 30. Hivyo miezi 42
ikizidishwa mara 30 ni sawa na 1260. Na kutokana na Ezekieli 4:6, siku 1260 ni
miaka 1260 ambayo pembe ndogo sasa, yaani upapa wa Rumi utatawala.
Kwa hiyo fungu hilo la Ezekieli 4:6, linatupatia ramani au
mwelekeo ufuatao wa Danieli 7:25 katika chati ya kiunabii hapo chini.
SIKU 1= MWAKA 1. Katika unabii (Ezekieli 4:6.)
Muda wa Kiunabii
|
Miaka
|
Miezi
|
Siku
|
Miaka halisi.
|
Wakati
|
1
|
12
|
360
|
360
|
Nyakati Mbili
|
2
|
24
|
720
|
720
|
½ Wakati
|
½
|
6
|
180
|
180
|
Wakati, Nyakati mabili,
½ Wakati
|
3½
|
42
|
1260
|
1260
|
Na je! Historia inasemaje kuhusu jambo hili? Je! Kuna uthibitisho
wowote kuwa Kanisa la Roma liliwatesa watu wa Mungu kwa muda wa miaka 1260?
“Vigilius…. Alikikalia
kiti cha upapa mnano mwaka 538 BK
chini ya ulinzi mkali wa kijeshi wa Belisarius.” History of the Christian Church, Vol. 3. p. 327.
|
Je!
Vigilius ni nani? Je! Alikuwa hata ni Mkristo?
“Pale falme kumi za Rumi zilipoanguka,
kulikuwa na mfalme mmoja aitwaye Justinian ambaye aliogopa sana kugawanyika
kwa ufalme wake. Alikuwa na Jenerali mkuu wa jeshi aitwaye Belisarius katika utawala wake ambaye alibuni naye mipango wakati wa vita iliyopelekea machafuko ya kuanguka kwa Rumi. Waliamua kuwa kama wataweza
kuingia katika mji wa Roma wataweza
kumwondoa askofu wa Roma ili kwamba wapachukue jambo litakaloweza
kuruhusu mfumo mpya wa ROMANI
Katholiki kusimamishwa. Walihitaji mfumo huu kwa sababu walifikiri hawatakuwa
na nguvu zaidi za kisiasa za kuwathibiti watu. Hivyo walibuni mpango kwamba
wawapatie utawala wa kidini na kisiasa pia. Hatimaye siku moja wakati
Belisarius anapambana, askofu wa Roma
alitangaza kuwa hataweza kuruhusu mapambano yoyote katika mji wake. Askofu
huyo alikuwa anawapenda watu wake na akaendelea kufunga mageti na kukataa
vita yoyote ndani ya mji isipokuwa iwe nje. Pambano la siku hiyo hakika
lilikuwa la aina yake. Walifanikiwa kumrudisha
Belisarius na majeshi yake nyuma kwenye kuta zilizokuwa zimebaki za mji wa Roma. Hilo liliondoa
matumaini. Ilionekana kana kwamba Belisarius anapotezwa kabisa. Hivyo
Belisarius alituma ujumbe wa haraka kwa mkuu wake Justinian ukisema “tuokoe!” Mke wa Justinian alikuwa
ni Mkristo ambaye alikuwa ni rafiki wa askofu wa Roma. Hivyo Justinian
alimwomba sana mke wake aongee na askofu wa Roma na amsihi kufungua mageti
ili Belisarius na wenzake waingie katika mji. Kutokana na heshima kati ya
mama yule na askofu, Salverius wa Roma
alifungua mageti ya mji na kumruhusu Belsarius na jeshi lake kuingia
ndani kuchunguza maisha yao.
Justunian na Belsarius walikuwa wamekwisha kukubaliana kuwa pindi
watakapofanikiwa kuingia ndani ni lazima kumwondoa askofu wa Roma. Kwa hiyo
walipoingia tu ndani kwa hakika walitimiza mipango yao.
Walifanikiwa kumwondoa askofu na wakamweka mtu wao waliomtaka Vigilius ambaye hata hakuwa Mkristo akakikalia kiti cha askofu na siku hiyo
akatangazwa kuwa ni papa. Unabii wa Ufunuo 13:4 ulitabiri hilo.
Katika mwaka 538 BK ni mwaka rasmi ambao kanisa la Romani Katholiki lilianza.”
Generalized Information taken from Hope
Beyond 2000 Video series “Rise of the
little horn of Daniel 7” – Kenneth Cox
|
Ushahidi wa kihistoria huonesha kuwa upapa ulianza kutawala rasmi mwaka 538 BK,
juu ya amri ya Justinian, na chini ya ulinzi wa jeshi la Belisarius. Na
Biblia husema pembe ndogo itatawala
miaka 1260 timilifu kabla haijapata jeraha la mauti. Sasa hili ni jambo tu la hesabu ya kawaida tena iliyo
rahisi. Na ni njia pia ambayo Mungu wetu
anatatukuzwa. Kama unabii huu ni sahihi,
miaka 1260 baada ya mwaka 538 BK, pembe
ndogo lazima ipokee jeraha la mauti na kupoteza nguvu yake.
Kama ukiongeza miaka 1260 kwenye mwaka ule ambao kanisa la Romani
Katholiki lilipoanza, ambao ni 538 BK, yaani 538+1260 kwa hakika utafikia
kwenye mwaka 1798 BK. Kwa mujibu wa
Biblia tunaambiwa kuwa utawala wa kwanza wa pembe hiyo ndogo, au sehemu ya
kwanza ya utawala wa hiyo pembe ndogo utakwisha baada ya miaka 1260 ambayo
huangukia mwaka 1798 BK. Je! Mwaka 1798,
upapa ulipata jeraha la mauti?
JIBU NI NDIYO! SIKILIZA!!!!!!
Mwezi February tarehe 10 Napoleon Bonaparte katika mwaka 1798 BK, alimtuma Jenerali Louis
Alexander Berthier, akiwa na
jeshi lake akavamie mji wa Roma, Italia.
“Mwaka 1798 BK, Jenerali Berthier aliingia Roma kukomesha serikali ya kipapa
na kuanzisha serikali isiyohusiana na dini” – Encyclopedia Britannica
1941 edition.
|
Hiyo ni miezi 42 halisi ya
kiunabii, au miaka 1260, au wakati, nyakati mbili , na nusu
wakati baada ya upapa kuanzisha utawala wake wenye nguvu na kwamba papa
atapata jeraha la mauti.
·
Danieli 8:9, “Na katika
moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa
kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.”
Kama tulivyokwisha jifunza vigezo vya kuitambua pembe ndogo katika
Danieli 7, tunajua kuwa pembe ndogo huwakilisha
mamlaka ambayo inahusiana sana na jina la ufalme wa Rumi . Uhalisia ni
kwamba, ulipopokea uwezo kutoka kwa ufalme wa Rumi, hata upapa nao pia uliitwa
“Papa wa Rumi” hadi sasa. Ongeza na kanisa nalo linaitwa “Kanisa la Romani
Katholiki”. Pembe ndogo hakika nayo ilitokea kama pembe kumi, ilizuka moja kwa
moja kutoka kwenye mnyama wa nne, ambaye
tayari tumejinza huwakilisha ufalme wa Rumi.
Sasa… nini kinachofuata?
·
Daniel 8:10,11 “Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha
chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga.
Naam, ikajitukuza
hata juu yake aliye mkuu wa jeshi
hilo, ikamwondolea sadaka
ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake
pakaangushwa chini.”
Kwa hakika upapa ilijitukuza hata juu ya Mwenyezi Mungu.
Ukweli ni kwamba upapa
ulijikweza kuwa ndio mkuu wa majeshi aliye juu ambaye kimsingi ni
Yesu.
Na sadaka (dhabihu) ya kuteketezwa ya daima kama ilivyoelezwa hapa
ni nini?
“Kisha niliona kuhusiana na “Dhabihu ya
daima (Danieli 8:12) kwamba Neno “Dhabihu” lilitumuwa kwa hekima ya wanadamu,
wala halihusiani kabisa na sentesi, na
kwamba Bwana alitoa usahihi wake kwa wale waliotangaza ujumbe wake wa hukumu.
Wakati umoja ulipoendelea, kabla ya mwaka 1844, karibu wote waliungana katika
mtazamo sahihi wa neno “ya daima”.
Lakini katika machafuko tangia mwaka 1844 mitazamo mingine imekuwa
ikishikiliwa, na giza na machafuko,vikafuata…” Maandiko ya Awali, uk
74-75
“Ya daima” humanisha inayoendelea, au
kudumu, lakini isiyo rejea kwa ile
sadaka ya kuteketezwa ya daima
ya Kristo au huduma yake ya daima. Hiyo inarejea kwa upagani kama
waanzilishi wanavyoamini.
Shetani
hutumia upagani hasa Rumi ya kipagani
“kuendelea” kuwatesa na kuwaua Wakristo, na alipoona kuwa jambo hilo
lilipelekea kukua kwa kanisa la Mungu, alibadili mpango wake wa kundelea kuua
Wakristo. Jukumu kubwa alillofanya ni kuwafanya Wakristo na wapagani kuungana
taratibu jambo lililo potosha imani ya kweli. Kisha aliwatumia wakristo hao
waliopotoka kuziamini imani za kipagani, na kuwatesa ndugu zao wenyewe walio
kataa kukubaliana na mafundisho hayo ya kipagani, ila waliobaki waminifu kwa
Mungu. Ibada ya sanamu ilikubaliwa kuwa ni sehemu ya ukristo, na ukweli
halisi ukakataliwa. Soma , Pambano
Kuu, (sura ya 2).
Kwa hiyo upagani ulipenya taratibu lakini
kwa uhakika chini utawala wa upapa wa Roma kwa kusaidiana na mfalme
Constantine, walifanikiwa hata kuweka sabato bandia yaani Jumapili.
Tangia mwaka 34 hadi 321 BK, upagani ( Rumi
ya kipagani) ilitawala. Katika mwaka 321, mfalme mmoja mpagani aitwaye
Constantine alisimamisha sharia ilikataza kufanya kazi siku ya Jumapili
isipokuwa shughuli ya kilimo tu. Sharia hiyo ilisomeka hivi; “ Siku ya jua
iliyo ya heshima hebu mahakimu na watu wanaoishi katika mji wapumzike, na
sehemu zote za biashara zifungwe. Na wale walio nje ya mji wanaojishughulisha
na kilimo hao wataruhusiwa kisheria kufanya hivyo; kwa sababu wakati
mwingine siku zingine huwa hazifai kwa
kupanda nafaka na mzabibu; kwa kupuuza muda husika wa kupanda mazao hayo,
fadhila ya mbinguni itapotezwa”.- source Book fo Bible Students, p.
578-80.,pia – “History of the Chriatian Church” vol 3, p. 380 by Philip
Schaff, 1893.
Baada ya mwaka 321 BK, upagani uliungana
taratibu na Ukristo kuabudu Jumapili na baadaye mnamo mwaka 508 BK Ukristo ulimezwa kabisa.
Mnamo mwaka 508, Clovis—mfalme wa “Franks”
(ambayo baadaye ilikuwa Ufaransa) alijiunga na Ukatholiki, na kuwashinda
Wagothi, (Goths= ni watu walikuwa wameitawala ngome ya Rumi au Ufalme wa Rumi
tangu karne ya 3 hadi ya 5). Jambo hilo halikuipatia upapa mamlaka meneo ya
mashariki tu, bali hata magharibu pia. “Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya
kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu
litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini.Heri angojaye,
na kuzifikilia siku hizo elfu na mia tatu na thelathini na tano.” Danieli
12:11-12.
“Ya daima” iliondolewa na upagani na
kuwekwa Jumapili kama siku ya kuabudu, na “chukizo la uhalibifu”(upapa wa Roma, na sabato
bandia) ikawa imesimamishwa, hapo sasa ndipo mwanzo wa siku/miaka 1290 na
1335.
Chanzo:- Let there be Light ministries
(Prophecychart, Item #9 & 10)
|
Kwa maelezo zaidi
kuhusu namna mafundisho ya uongo au wakristo na wapagana walivyo fungamana,
soma ;
Pambano
Kuu, sura ya 3,”Giza la Kiroho Katika Kanisa la Kwanza”.
Cardinal Wiseman’s
Lectures on “The Real Presence” lecture 8,sec.3 para 26.
Wylie – History of
Protestantism, Book 1, chapter 4.
Vatican ilijaribu kuharibu kazi ya Kristo.
|
|
Mwaka
|
Tukio lililotokea
|
585
|
Kubadiri Sabato ya kweli ya
siku ya 7 kwenda siku ya 1
|
593
|
(Purgatory); mtu kuteseka
huko ahera kwa dhambi alitotenda ili atakasike kabla ya kuingia mbinguni.
|
600
|
Ibada ya wafu (kuombea
waliokufa)
|
750
|
Papa azungumze badala ya
Mungu
|
788
|
Ibada ya sanamu, msalaba,
mabaki kama mafuvu ya watu nk.
|
995
|
Kutakatifisha majina ya wafu
|
1050
|
Huduma ya kimizimu, yaani
misa(mass), iliyowekwa baada ya kuondolewa mezw ya Bwana
|
1190
|
Kusali rozari
|
1190
|
Kuuza kadi za kutubia
|
1215
|
|
1215
|
Kutubu dhambi kwa padri.
|
1229
|
Halimashauri ya Valencia
iliweka Biblia kizuizini
|
1545
|
Utamaduni ukawekwa juu ya
Biblia
|
1546
|
Vitabu vya uongo vya kubuniwa
viliongezwa kwenye Biblia
|
1854
|
Dhana ya kumweka Mariam kuwa
mama wa Mungu na asiye na Dhambi
|
1870
|
Papa atangazwa kuwa hana
dosari katika mambo ya kidini
|
1894
|
Mariam afanywa kuwa naye ni
mwokozi,mpatanishi na mwombezi wa watu.
|
Pembe ndogo hukubali na kuthihilisha dhambi hadharani kama
Wakristo wanavyo mdhihirisha Kristo.
·
Danieli 8:12, “Na
jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya
makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na
kufanikiwa.”
Ile kufundisha kuwa watu
hupata haki kwa njia ya matendo badala ya haki kwa njia ya imani, upapa ulishambulia
kazi ya Yesu ya sadaka ya kuteketezwa. Pia upapa kuangusha kweli hata chini, kwa
kuleta mafundisho yanayopingana na Biblia kama hayo yaliyoorodheshwa hapa juu
na madang’anyo mengine kama ya maisha ya milele katika kuzimu, kubatatiza
watoto wadogo hii yote ni kupotosha watu na kupinga kweli ya Biblia. Hayo mafundisho ya uongo yametoka
upaganini ili kuchukua nafasi ya Biblia kama unabii unavyosema kuwa ilikuwa
mpango wa Shetani kufanya hivyo. Shetani siku zote amekuwa na lengo la
kuangusha kweli ya Mungu kama alivyofanya pale bustani ya Edeni; Mwanzo 3:4.
Agizo la Mungu ni kuwa wakila matunda ya mti waliyokatazwa hakika watakufa,
lakini kauli ya mwovu Shetani ikawa “…Hakika
hamtakufa”.
Mafundisho yote ya uongo ya kanisa la Romani Katholiki yameangusha
kweli ya Mungu hata chini; cha ajabu zaidi ngudu msomaji ni kuwa “imefanikiwa” kutenda mambo yake yote ya upotofu.
Danieli 8:16,23 “Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto
Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya. Na wakati
wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali,
afahamuye mafumbo, atasimama”
Katika fungu hili la kiunabii tunaona kuwa Gabrieli anathibitisha
kwamba kiongozi wa mamlaka hii ni “ mfalme
mwenye uso makali” na mtu atakayefahamu “mafumbo”.
Je! Hili siyo kanisa la Romani Katholiki lenye uso mkali? Je!
Halijajigamba lenyewe kuwa liko hivyo? Pia, kanisa hili halikujigamba lenyewe
kuwa ndilo lifahamuye mafumbo?
Historia iatuelezaje!
Ushetani kugundulika Vatican
Watu wawili maarufu wa kanisa wametangaza
“Ushetani unatendeka Vatican!”
“Wiki za hivi karibuni, moto mkali umekuwa ukiwaka Italia. Utata
umetatuliwa na kauli za askofu mkuu Emmanuel Milingo, ambaye alitoa madai
rasmi kuwa shughuli za kishetani zinatendeka ndani ya Vatican.
Alipoulizwa na vyombo vya habari vya
Italia kuhusu madai hayo aliendelea
kusema kuwa madai hayo ni sahihi. Askofu aliamua kuchagua Mkutano wa
Kimataifa juu ya Amani ya Ulimwengu ulifanyikia Roma Novemba 1996 ulio andaliwa na gazeti
la ‘Fatima Crusader’ kama jukwaa la kwanza la kuufanya uma kufahamu madai
hayo”. –Sunday, February 28, 1999 www.fatima.org/satanism.html
|
Hakuna mahali popote duniani au kitu chochote tunachoona kuwa na uhalisia kinachofunuliwa
kama pembe ndogo isipokuwa ni upapa wa
Romani Katholiki. Je! Hii ni kwa bahati mbaya? Au kuna nguvu kutoka nje
inayotenda yote haya?
·
Danieli 8:24, “Na
nguvu zake zitakuwa nyingi mno, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe; naye
ataharibu kiasi cha kustaajabisha watu, na kufanikiwa, na kutenda apendavyo;
naye atawaangamiza hao walio hodari na watu watakatifu.”
Nguvu za upapa kimsingi si kwa uwezo wake, ni kutoka nje. Bila
shaka zilitoka kwanza kwa Shetani,ambaye
hapo awali ndiye aliye toa uwezo wake
kwa ufalme wa Rumi, na baadaye ufalme wa Rumi ukampa Papa wa Roma nguvu nyingi
na mamlaka mnamo mwaka 313 BK.
Constantine mtawala wa Rumi aliongoka
na kuwa Mkristo lakini akachanganya Ukristo na upagani; hivyo alifanya uongofu
bandia. Jambo hilo lililipeleka kanisa katika nafasi kutokukataa wala kuhoji
matakwa ya mfalme huyo kulingana na mamlaka aliyokuwanayo. Yesu
alilitahadhalisha kanisa kuwa lijihadhali na mbwa mwitu wanaokuja katika vazi
la kondoo. Wengi wetu kwa kweli tunayo
macho sasa yakuona hawa mbwa mwitu wakali, tumshukuru Mungu kwa kutufunulia
unabii. Lakini jambo baya sana ni kwamba, mabilioni ya watu kwa sababu ya
kushupaza mioyo yao na kutokufuatilia uhalisia kama huu wa kiunabii, tena hata
hawakotayari kusoma Biblia wakidai kuwa ni kitabu chao tu, wako hatarini
kutekwa na hila za setani na hata kupotea milele. Watatoa udhuru gani siku ile Bwana
atapokuja? Pia kwa wale waliopewa ujumbe
wakachagua kuukataa kwa kufuata misimamo ya madhehebu, watatoa udhuru
gani?
Kuanzia mwaka 313 BK hadi 538 BK, nguvu ya upapa ilidhihirika
wakati ilipounda ushirika na mataifa yanayoizunguka ambayo hapo awali ndiyo
yaliyokuwa yanaunda Rumi iliyoanguka. Matokeo ya ushirika huo ndio kiini cha
kurudi kuwa na nguvu tena kama tuonavyo sasa.
Kuchanganya ukristo na upagani katika kanisa imesababisha mabilioni ya watu kwenda kaburini
wakiwa wamegubikwa na giza la mafundisho ya uongo. Kama ilivyokuwa mwanzo
kanisa hili hadi sasa limeendelea kupuuza ukweli wa Biblia. Zaidi ya watu
bilioni 1 hudai kuwa Ukatholiki ndio imani yao na ndiyo imani ya kwanza kuwepo. Na mpaka sasa ndilo dhehebu lenye idadi kubwa ya watu
duniani kuliko dhehebu lolote lile. Na
wakati ule wa tarehe 26th
June , 2000 wakati Papa alipokuwa kiongozi Muungano
wa Makanisa, mabilioni zaidi wamejiunga na imani hiyo iiliyojaa
makufuru.
·
Danieli 8:24, “Na nguvu
zake zitakuwa nyingi mno, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe; naye ataharibu
kiasi cha kustaajabisha watu, na kufanikiwa, na kutenda apendavyo; naye
atawaangamiza hao walio hodari na watu watakatifu.”
Sambamba na kwenda kinyume na Kristo “Mkuu wa wakuu” na kinyume cha
wateule Wake. Unabii unasema upapa utawaangamiza watu hodari nje ya kanisa la Kristo ili kufanikisha
malengo yake. Kampeni ya kupinga Uislam, karne ya 11 hadi ya 13 na mauaji yaliyofanyika yalitendwa na chombo hiki kiovu. Na Baraza la Hispania dhidi ya kile ambacho Roma
hukieleza kama wazushi lakini Biblia huwatambua kama Wakristo, tunaona liliua
Wakristo wengi kwa ajili ya imani yao katika Kristo. Mbaya zaidi ni kwamba
tumekwisha kushuhudia mifano michache ya mipango yake miovu. Roma imetenda
mambo mengi sana kwa kujificha zaidi hata
ya yale tutakayoweza kufahamu. Ukweli ni kwamba sababu ya kufahamu
matukio maovu yanayofanywa na Roma,
Mungu anahitaji tifumbue macho mara tunapo linganisha matukio hayo na unabii
tunaojifunza ili yuwe na maamuzi kabla siku ya kuja kwa Kristo haijafika. Mungu
alijua kuwa histieria itarekodi kila kitu kitakachofanywa na Roma, na Anajua
pia watu wake watafahamu unabii kwa kulinganisha matukio hayo
katika siku za mwisho.
Asante
Yesu!
·
Danieli 8:25,” Na kwa
mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake
moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye
atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya
mikono.”
Tumshukuru Mungu aliye juu! Hii mamlaka mbaya ya pembe ndogo,itavunjika tena “bila
kazi ya mikono” ya mwanadamu yeyote
duniani. Yesu ndiye atakefanya kazi hiyo mwiso wa dunia. Kuvunjika huku siyo
pale miaka 1260 ilipotimia mwaka
1798, isipokuwa ni pale ilipotawala kwa mara ya pili baada ya
kupona jeraha la mauti, ambapo ndipo Kristo atakapokuwa amwrudi kwa mara ya
pili.
Je! Ni watu gani watakuwa washindi?
·
Danieli 7:27, “Na
ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye
juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka
watamtumikia na kumtii.”
Ama kwa hakika watakatifu wake Aliye juu ni wale tu waisikiao
sauti yake na kuitii. Ndio walio kubali
kufuata Maandiko matakatifu na kukemea
mafundisho ya uongo na mapokeo ya wanadamu. Ni wale tu walio itunza
imani ya Yesu na kushika amri kumi ndio
watakaopewa ufalme wa milele. Ndugu yangu ni muda wa kujihoji, ikiwa kanisa
ulilopo limekanyaga maandiko matakatifu au amri za Mungu kwa kufuata faida za kidunia,
fanya hima utoke ujiunge na kondoo wa Yesu kabla muda haujakwisha maana Yesu
anakuita ni vema kwako ukiitika.
Ufunuo 18:4, “Kisha
nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu
wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.”
Ninayo furaha kuu kusema kuwa unabii wa kuhusu pembe ndogo umeisha
kwa furaha. Mungu mwenyezi ataukomesha utawala wa kipapa na matendo yake yote
maovu, na kuanzisha utawala Wake usio na mwisho kwa wale wote walioisikia sauti
yake na kukubali wito wa wokovu. Roma na
mawakala wake wakatili wote wataangamizwa. Na wafuasi wa Yesu wataishi
Naye kwa furaha milele na milele amina!
Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi
nyote. Amina.
Habari zaidi kuhusu masomo haya;
Namba, +255758924982, +255714697526.
Facebook; Mwl Ndiku.
Habari, naweza kutumiwa mafundisho haha kwa njia ya email?
ReplyDelete