SIRI YA USHINDI.
"Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu."
Ndugu wapendwa Amani ya Bwana iwe pamoja nanyi!
Ushindi ni hatua inayopatikana baada ya mapambano,vita,mikikimikiki katika swala fulani,nk;na Mara zote aliyeshinda katika swala fulani lazima awe na siri fulani,iliyokuwa tegemeo lake!
Japo katika maisha haya kuna mategemeo mengi,wengine wakitumainia nguvu zao,wengine nguvu za giza,n.k, lakini katika hayo yote ni ushindi wa kitambo tu,ushindi huo unafurahiwa muda ,na muda baadae ni huzuni!
Mfano atokee mtu awe tajiri katika Mali za dunia,miaka kadhaa,kisha mwisho wa siku awe masikini wa kuomba-omba,bila shaka huyu mtu atakuwa Mwenye huzuni saana!
Katika somo letu tujaribu kuangaza wale watakosifiwa mbinguni kuwa washindi, nini kilichowapa ushindi huo udumuo siku zote?
Karibuni
Tuangaze kwanza vita waliyokabiliana nayo,ndipo tuweze kuona pia nini kilichowasaidia kupata ushindi huo!
a) "Mungu aliruzuku nuru kubwa kwa watu wake,lakini hatuko chini ya kivuli cha kutokutenda dhambi"CH 586
Kwa fungu hilo hapo juu twaona kuwa Pamoja na Nuru tuliyopewa,haituweki mahali tusipoweza kujaribiwa na ibilisi,kumbe kwa mantiki hiyo,tuko mapambanoni, yatuupasa tushinde!
b) "Moja ya mitego mahususi ya Shetani,ili kuwashinda watu wa Mungu,ni kubomoa mageti yanayowatenga na dunia"DA398 Soma Zaburi pia 11:3 "Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini?" Ieleweke kuwa Shetani kazi yake nyingine ni kukata matawi ya matumaini tulioegemea,na matokeo anakusudia tuangukie duniani(mitegoni mwake)
c) "...Hivyo Lusifa huongeza juhudi Maradufu katika mbinu za kutaka kukwamisha kazi ya upatanisho.Anakusudia kushikilia roho katika giza na kutokutubu mpaka huduma ya Ukuhani wa Kristo imalizike na pale patakapokuwa hakuna kafara tena kwa ajili ya dhambi;hilo ndilo kusudi lake"GC518.1
Cha kushangaza,wale waliodumu dhambini,Kristo atakapo kuwa amemaliza kutia muhuri,Shetani kwa kebehi na kejeli kubwa atuambia hao "Nendeni nanyi mkajiaandae Mwokozi wenu anakuja"!!!!! Ni huzuni kiasi gani??? Fananisha na Mathayo 25 (wanawali wapumbavu)
d) "Kwa kadiri tufani ikaribiavyo, watu waliojidai kuwa waumini katika ujumbe wa malaika wa tatu, lakini hawakutakaswa kwa ile kweli, watauacha uamini wao na kujiunga na upande wa upinzani."Pambano Kuu 196— ni shambulio la kikomando,kwamba wewe uwe muumini ktk kundi lolote LA kidini,lakini ibilisi akikufanya usienende sawasawa na ukweli,anajua utakuwa wake,haijalishi leo unamshambulia kiasi gani!
Bila shaka kwa hayo,hatuna mbinu ya kushinda,isipokuwa kwa nguvu za asiyeshindwa kamwe(Kristo simba wa shina la Yese)
USHINDI U KATIKA UWEZA WA DAMU YA KRISTO.
★ "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;" Yohana1:12.
Kwa kauli hii ya Yesu,yaonyesha kuwa wote tutakaomuamini,atatuwezesha kuingia katika utii sawa na malaika wa mbinguni!!! Ni shangwe iliyo je! Hallelujah
★ "Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa." Efeso4:8
Kwa kushinda kwake tulipata uwezo wa kushinda pia,katika yeye tu makomando wa vita,yeye akiwa amiri-jeshi,tutateka ngome za shetani na kuziangusha na baada ya hapo tutaitwa washindi hodari wa vita!
MAADUI WA MUNGU NA NGOME ZA KUANGUSHWA.
"Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami."
Waweza kuwa mwanafunzi machachali wa Kristo kama Petrol,lakini utashangaa kuambiwa"toka nyuma yangu eee shetani"
Ni kwakuweka roho yako mbali na Kristo ndivyo unavyojiweka katika uadui na Kristo, haijalishi mwili na Mali zako ziko kanisani!
"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili;(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;"2 Korintho5:3-5
Nawatakieni tafakari njema na kuamua Kristo afanye vita ndani yetu aangushe tamaa za uzinzi,ugomvi,ubinafsi,kiburi ili Sura ya chapa ya Tabia ya Uungu ionekane ndani yetu!!
Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi
nyote. Amina.
Habari zaidi kuhusu masomo haya;
Namba,+255753181739+255758924982, +255714697526
Facebook; Mwl Ndiku
No comments:
Post a Comment